Loading...

Esma Platnumz Amkingia Kifua Wema

October 19, 2018 at 10:17
Esma Platnumz Amkingia Kifua Wema
Loading...

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kumkingia kifua Wema Sepetu kutokana na sakata linaloendelea hivi sasa Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya juzi Wema alimtambulisha mpenzi wake mpya ambaye amedai ndiye atakuwa mume wake mtarajiwa lakini moja kwa moja hali ilibadilika kwani mwanaume yule ameshawahi kumtukana Wema.

Loading...

Mashabiki mbali mbali wa Wema walimshauri avunje Mahusiano na mwanaume yule na wapo hata Mastaa Wenzake ambao walimshauri atulie kwani mwanaume yule tayari ana wake wawili.

Lakini Esma ameibuka na kumpa sapoti Wema na kulpongeza kwa maamuzi  yake na kumtaka kufanya  kile ambacho moyo wake umeridhia na kama anataka Kuolewa na yule mwanaume basi ruksa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma ameandika maneno haya kwenda kwa Wema:

Go go Mu forever wiii cha muhimu ukiwa naye uko happy, ifike mahali tuheshimu hisia za watu jamani tutapangiana maisha mpaka lini? Insta imekuwa sehemu ya watu kutuchagulia maisha watu tuishi vipi khaaa Wema ngoja na mimi nikitoe kibabu changu”.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…