Fahamu mahusiano ya Madee na Rayvanny nje ya Muziki

Msanii wa Muziki, Madee amefunguka kama kuna mawasiliano kati yake na RayVanny baada ya kuwahi kufanya nae kazi Tip Top Connection alipoanzia.Madee anasema kuwa hata kama waliwahi kufanya kazi pamoja lakini inafika sehemu kila mtu anakuwa na maisha yake  na lazima maisha yaende.

Mahusiano ya way back na sasa hivi hayawezi kuwa sawa, mimi plan zangu nikuona mtu anaendelea kwenye maisha yake yaani anatimiza kile anachokiota, Mwanzo lazima mahusiano yawe karibu sana kwasababu tunalala wote tunaamka wote tunawasiliana muda wowote,” alisema Madee.

Lakini pia anaonezea na kusema  kuwa kwa level waliofikia haiwezi kuwa kama zamani kwamba wanaweza kupigiana simu na kuanza kuombana pesa kama zamani walipokuwa wakiombana hata 2000 kwa ajili ya kula.

download latest music    

Kwasasa hivi lazima kuwe kuna vitu vinapungua,kwasababu sasa hivi hawezi kunipigia simu kuniomba 2000, 3000 kwasababu anayo, sasa hivi hawezi kunipigia simu kuniomba gari kusema aende sehemu fulani kwasababu analo lakini heshima bado iko pale pale ananiheshimu na anaheshimu kila kitu kilichotoka kwangu hakuna kitu chochote kilichobadilika.”

Kwasasa Rayvanny ni msanii aliyesainiwa kwenye lebo ya WCB Wasafi iliyo chini ya msanii Diamond Platnumz.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.