Faiza Ally Alilia Umoja na Ushirikiano Kwenye Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally amefunguka na kuendelea kulia na Bongo movie huku akiwa sihi wasanii wenzake wazidishe umoja na ushirikiano baina yao.

Faiza Ally ameongea hayo huku akilihusisha tukio la kusikitisha lililotokea siku chache zilizopita baada ya kifo cha Agnes Masogange na ushirikiano wasanii wote walionyeshana.

download latest music    

Faiza amewataka wasanii wa bongo movie kuwa na umoja na ushirikiano kwenye sanaa na kufanya filamu kama walivyokuwa kwenye msiba ambapo amesisitiza kama Ikiwa hivyo basi ni wazi kuwa sanaa hiyo itafika mbali.

Faiza alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika ujumbe huu:

Tunaishi kwa kujifunza na mara nyingi mitazamo ya nje sio halisi, naomba nimpongeze IreneUwoya kwa kuwa rafiki mwema a special kipindi hiki, nimemuona akishiriki na kwenye utulivu sana yaani kasimama kama rafiki na hivi ndio inavyo takiwa, yaani jambo linapo kufika la mtu wa karibu sio kulia sana au kupoteza fahamu lazima usimame ujue hatma ya mwenzio kwanza.

Nahisi Bongo Movie tuna vitu vikubwa sana wote kwa pamoja lakini sijui tunakosea wapi, maana kwa ushirikiano huo huo wa msibani, urudi kwenye kwenye kazi naamini kuna hatua kubwa sana tutapiga, nisema tu mpo vizuri sana, nyinyi ni wa maana sana“.

Agnes Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao Mbeya ambako alizikwa jana Aprili 24, 2018 kijijini kwao Utengule, Mbalizi

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.