Faiza Ally Amemtolea Povu Zito Mzazi Mwenzie Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo Faiza Ally amemjia juu tena na kumwagia povu zito mzazi mwenzie, mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’.

Faiza na baba mtoto wake Sugu wamekuwa hawana maelewano yoyote linapokuja swala la malez na matunzo ya binti yao Sasha. Faiza amekuwa akitumia mitandao ya kijamii mara kwa mara kuelezea hisia zake za kuchukizwa kwa vitendo vya Sugu kukataa kumlea mtoto wao huku Sugu akisisitiza kuwa Faiza ndio anakataa kumpa nafasi ili amuhudumie mtoto wao kwa nafasi leaning anamuwekea masharti mengi sana.

download latest music    

Siku ya Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza Ally alifunguka yafuatayo kuhusiana na kukerwa na vitendo vya mzazi mwenzie Sugu na kumrushia povu hili;

Wewe baba Una roho mbaya Sana na Inshallah MMungu atakulipia hata baba yako yule Mzee Mtambuzi aliye kuwa anamsaidia mwanao na kunipa faraja japo ya maneno umemjaza maneno sasa hataki hata kuwasiliana na Mimi khaa! Una haya kweli unanizibia mpaka unaziba kwa mwanao? Wallahi Mungu akulaani ulipo usije kuwa na furaha milele kama mbavyo unanikosesha amani kwenye maisha yangu na mwanangu. Hivi viongozi hamliobi hili jitu kwamba halifai kuwa mfano bora kwa jamii? Mfano gani mnaonyesha kwa jamii najua unaweza hata kuniua kwa ubaya ulionao juu yangu panini sikuogopi Niue tu na mimi nikapumzike kwa ushenzi wako wa chini kwa chini…Kwa eoho mbaya unayonifanyia unaweza hata ukamuua mwanangu ili uniumize”.

Baada ya kuandika maneno haya watu walimjia juu  na kuamua kufuta na kuhaidi kuwa hataandika tena Maneno yoyote kuhusiana na Sugu.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.