Faiza Ally awajia juu wanaozusha kuwa Sugu ni baba wa mtoto wake mdogo

September 13, 2017 at 12:42
Faiza Ally awajia juu wanaozusha kuwa Sugu ni baba wa mtoto wake mdogo

Mwanamitindo machachari Faiza Ally amewajia juu wale wote wanaozusha na kudai kuwa baba wa mtoto wake wa kwanza, Mheshimiwa joseph Mbilinyi  maarufu kama Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya mjini pia ni baba wa mtoto wake mchanga anaitwa Lil junior

Faiza na Sugu ambao walikuwa wapenzi wa muda mrefu waliachana miaka michache iliyopita lakini tangu wametengana wamekuwa wakigombana kwenye mitandao ya kijamii huku Faiza akimtuhumu mzazi mwenzie huyo kwa kukataa kumtunza binti yao Sasha, mpaka kufikia hatua ya kwenda kupelekana mahakamani. Ni wazi kuwa Faiza na mzazi mwenziye huyo hawana uhusiano mzuri lakini Faiza amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuonyesha hisia zake na kumwambia Sugu kuwa bado anampenda na angependa warudiane.

Kumekuwa na  tetesi mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kuwa mtoto mpya wa Faiza aliyejifungua hivi karibuni ni mtoto wa Sugu, hii ilitokana na kuwa Faiza alikataa kumtaja hadharani baba wa mtoto wake.  Pia watu wamedai kuwa Sugu na mtoto huyo wamefanana. Lakini kwa kupitia ukurasa wake wa instagram Faiza alifunguka yafuatayo.

 ”Huyu mtoto jamani ana baba ake kha sema nishashasema Sugu akitaka mtoto nampa na ninavyomfyatulia kiroho safi ntaprinti tu sio kesi si mnajuaga bado nampendaga mwanangu Lil junior huyu sasa umepewa baba za 4 ama kweli your born to be a star kid”.

Mpaka sasa Faiza na Sugu hawana uhusiano mzuri baada ya Sugu kumtuhumu Faiza sio mama bora na kumpeleka mahakamani akitaka amchukue mtoto wao Sasha na Faiza kuntuhumu Sugu kumkataa mtoto wao na kutotoa pesa za matumizi.

Leave a Reply

5 Comments on "Faiza Ally awajia juu wanaozusha kuwa Sugu ni baba wa mtoto wake mdogo"

avatar
Sort by:   newest | oldest | most voted
Vida Fais
Guest
Vida Fais

His face like Mr Sugu 100%

Habiba Jaffari
Guest
Habiba Jaffari

Kafanana na sugu hamna kuficha

Jessica Mrisho
Guest
Jessica Mrisho

Unanikoshaga kiukwl wewe dada

Farida Aisha
Guest
Farida Aisha

jmn watu huwa hawa achani huyu Sugu mbuna tu

Dorothy Rita
Guest
Dorothy Rita

Mtoto wa rais wa Mbeya huyu look alike kabisa

wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.