Faiza Ally- Bado Nampenda Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Faiza Ally amefunguka na kudai bado anampenda Baba wa Mtoto wake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Sugu na Faiza walikuwa kwenye mahusiano miaka kadhaa iliyopita lakini pamoja na kuachana wamendelea kukamata headlines kwa maugomvi yao ya mitandaoni.

download latest music    

Faiza pamoja na kumdhalilisha Sugu Mara kwa Mara kwenye mitandao ya kijamii huku akimtuhumu kwa kumtelekeza Mtoto wao bila huduma yoyote.

Pamoja na kukosa maelewano Faiza ameibuka na kudai kuwa bado anampenda sana Sugu na amejaribu kuwa na wanaume wengine lakini ameshindwa ikiwemo kuzaa na mwanaume mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza ameandika maneno haya:

Baada ya kuandika maneno hayo mashabiki wengi walimjia juu wakidai kwa kuandika hivyo anakuwa anamkosea heshima mke wa Sugu ambaye hivi sasa ni mjamzito wanatarajia kupata Mtoto wao wa kwanza.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.