Faiza Ally: Gabo Sio Aina Ya Mwanaume Naweza Kuwa Naye

Mwanamitindo na muigizaji wa bongo movie asiyeishiwa vituko Faiza Ally ameibuka na kudai kuwa muigizaji wa bongo movie Gabo siyo aina ya mwanaume anayeweza kutembea naye wala kuzaa naye.

Baada ya Faiza kuzaa mtoto wake wa pili anayeitwa Li bila kumtambulisha baba mzazi wa mtoto huyo watu wengi wamekuwa wkijiuliza je ni nani baba mtoto wake? Moja kati ya watu ana ukaribu nao ni mwigizaji Gabo ambaye hata amewahi kuigiza naye filamu inayoitwa ‘baby drama’ na zaidi ya hapo amewahi kusema huko nyuma kuwa amewahi kuwa mpenzi wake hivyo watu wengi hasa mashabiki zake kwenye mtandao wa jamii instagram wamekuwa wakimtaja mwigizaji Gabo kuwa ndiye baba wa mtoto hadi kufikia hatua ya kumfananisha na kudai kuwa wanafanana.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza alifunguka kuwa Gabo sio baba wa mtoto wake na wala hajaona mwanaume wa kutembea naye Tanzania kwa hivi sasa.

Ngoja niwaambieni ukweli kuhusu Gabo naona watu wengi mmeamini kabisa kuhusu Gabo! Ni hivi tulikua na kipindi cha Family love kinachorushwa na Clouds Tv na mimi na Gabo ni wanafamilia na mtoto wangu Li ilitakiwa akizaliwa iwe moja kwa moja familia ya ukweli hata ile posti niliyosema kama Gabo ndiye baba wa mtoto ilikuwa ni kukitafuta kipindi namna ya kujulikana, ukweli ni kwamba mimi na Gabo kwanza ni marafiki, pili ni kaka na dada, tatu ni tumefanya kazi mbili pamoja kwa hiyo katika mapenzi mimi na yeye hatujawahi wala hatutowahi zaidi ni mtu mwenye familia yake ana mke na watoto siwezi especially kwa mtu maarufu! kwa hiyo naombeni mtoe fikra zenu mana naona naitwa mrs Gabo na mtoto wangu juu mnamsema ni wake! hapana si wake. Mimi sina bwana Tanzania niko nalea tu halafu  pia kuwa na mtanzania kwa sasa hapana labda awe na quality ninazo zitaka mimi lakini bado sijaona”.

Alimalizia kufunguka Faiza ingawa mpaka sasa amegoma kumuweka wazi baba wa mtoto wake kwa sababu zake binafsi mwenyewe.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.