Faiza Ally: Siwezi Kumpeleka Mwanangu Akamuone Sugu Jela

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi na wala hana mpango wa kumpeleka binti yake Sasha aliyezaa na Sugu akamuone baba yake jela.

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Faiza wamezaa mtoto mmoja Sasha, na Faiza amedai kutokana na kutokuwepo maelewano kati yake na Sugu hategemei kumpeleka mtoto wao gerezani kumuona Baba yake.

download latest music    

Sugu yupo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya akitumikia kifungo cha miezi mitano aliyohukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Mchanganyiko Faiza aliulizwa endapo atampeleka mtoto wake jela kwa kipindi hiko alichofungwa Faiza alisema hawezi kumpeleka maana Sugu sio ndugu yake.

Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto akamuone gerezani kwa sababu kwanza siyo ndugu yangu, siyo rafiki yangu na siyo mpenzi wangu. Mapenzi yalishaisha zamani, amebakia kuwa baba wa mtoto, basi, hayo mengine siwezi kuyafanya kwa kweli“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.