Familia Ya Ndikumana Imempa Uwoya Baraka Zote Kuendelea na Maisha Yake ( Picha na Video)

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amekuwa katika kipindi kigumu sana kwani mara baada ya kufunga ndoa na mumewe Dogo Janja mume wake wa zamani Hamad Ndikumana alifariki dunia hali iliyozua utata kwani habari zilisema kuwa Uwoya alikuwa na ugomvi na familia ya marehemu mumewe hadi kufikia hatua ya kukatazwa kuhudhuria msiba.

Baada ya Uwoya kusafiri na familia yake kwenda Nyumbani kwa Ndikumana na familia yake nchini Rwanda alionekana kupokelewa na hata kuweka wazi kuwa tofauti na watu walivyokuwa wanadai kuwa wakwe zake walimshutumu kuwa kamuua mtoto wao lakini wameonyesha kumpokea vizuri na hata kulia naye na mwishoni wamempa baraka zote ili akaendelee maisha yake na mume wake mpya.

download latest music    

Tangu kifo hicho kitokee Uwoya hajaongelea sana bali aliandika maneno haya machache kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Mungu wewe ndio unajua moyo wangu ukinijua wewe inatosha…My trust is in you Gid.. R.I.P Baba Krish”.

Hizi ni baadhi ya picha na video zinazomuonyesha Uwoya akipewa baraka zote na familia ya Ndikumana huko nchini Rwanda:

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.