Familia Ya Ndikumana Yampokea Irene kwa Amani.

Kutokana na tetesi zilizokuwepo kuwa inawezekana Irene Uwoya ndie alisababisha kifo cha alikuwa mumewe kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana Kataut ambae  alifariki wiki iliyopita huku sababu kubwa ikisemekana kuwa ni ugonjwa wa moyo alioupata kwa ghafla huku  ikisemekana kuwa sababu kubwa ni kuwa na msongo wa mawazo aliokuwa nao amad kutokana na ugomvi  wa muda mrefu na mkewe huyo Irene Uwoya.

Irene alisafiri akiwa na mama yake kutoka Tanzania kwenda Rwanda siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuona kaburi alilozikwa mume wake huyo, huku baadhi ya watu wakiwa na wasiwasi kuwa inawezekana familia ya Ndikumana na mashabiki wake watakuwa na hasira sana na msanii huyo wa bongo movies.

download latest music    

Lakini baada ya Irene na familia yake kufika kule walipokelewa vizuri sana na familia ya Ndikumana na kusemekana kuwa familia hizo mbili zimesameheana kutokana na kuwa kifo kilishatokea na inabidi mambo mengine yaendelee.Pamoja na kwamba inasemekana kuwa mashabika walitaka kuifanyia fujo familia ya Irene Uwoya lakini familia ya Ndikumana waliwatuliza mashabiki hao kwa sababu wao kama familia wameshasamehe tayari.

Akisimuliza kwa undani moja ya watu walioambatana na  familia hiyo alisema kuwa ,zile tofauti walizokuwa nazo wameziweka pembeni, na mama ndikumana aliwaambiwa kuwa walishasamehee hivyo wakaanza kuombeleza upya kwa sababu mama irene alikuwa akilia sana na mpaka akawa hawezi kutembea.

Pia ,Mike Sangu ambae pia ni mmoja wa watu waliokuwa katika msafara huo ingawa wao walichelewa kufika msibani  kwa kuwa walisafiri na basi ,pia alithibitisha kuwa mama Irene, Irene na Krish walipokelewa vizuri walipofika Rwanda na kupewa ulinzi mzuri mpaka walipofika nyumbana na hapakuwa na fujo zozote zaidi ya kuombeleza katika msiba huo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.