Loading...

Gigy Money Afungukia Mahusiano Ya Mo J na Diva

October 12, 2018 at 18:29
Gigy Money Afungukia Mahusiano Ya Mo J na Diva

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuongelea uhusiano unaoendelea kati ya  Mtangazaji wa Choice FM Mo J na mtangazaji wa Clouds Fm Diva The Bawse.

Siku chache zilizopita kuna tetesi zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diva na Mo J ambaye ni mzazi mzazi mwenzake na Gigy Money wapo Kwenye Mahusiano.

Loading...

Tetesi hizo zilichochewa na video iliyosambaa kwenye social media iliyowaonyesha Wawili hao wakiwa katika mikao ya kimahaba na hivyo kuibua tetesi za uhusiano.

Tangu Gigy Money  ameachana na Mo J ameweka wazi kuwa hawana maelewano mazuri licha ya kumlea mtoto wao pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy amefunguka baada ya kuulizwa anajisikiaje baada ya kuona Diva Yupo Kwenye Mahusiano na Baby daddy wake ambapo alijibu:

Kawaida sana maaana sina mkataba nao, Hata wewe kipenzi unaweza ukapita naye kiroho safi”.

Lakini pia Gigy Money amesisitiza kuwa hawezi kurudiana Tena na Mo J na hata kuzaa naye Tena hawezi kuthubutu.

Share

Comments

  1. wakupendana wapendane tu

  2. gigy uko sawa kabiss

  3. Achana nao

  4. huyu diva mbona simpendi tu

  5. walisha achana kwahio sioni shida iko wapi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…