Gigy Money Agoma Kuolewa Kwa Mahari ya Milioni 5

Muuza nyago kwenye video “Video vixen” ambaye pia amegeuka kuwa mwanamuziki Wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu Kama Gigy Money, amejikuta akipiga kikumbo Bahati baada ya kugomea kuolewa kwa mahati ya shilingi milioni tano (5) kutoka kwa mwanaume aliyetaka kumuoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Gigy Money anayetamba na wimbo wake mpya Wa “Papa” alisema kuwa sio kwamba hapendi kuolewa lakini anachoangalia ni thamani yake ambayo Kama ni kuolewa baso atolewe mahari ambayo ni zaidi ya milioni tano.

download latest music    

Gigy Money alisema:

“Namshukuruç Mungu Bahati ya kuolewa ninayo lakini, watu wanashindwa kutekeleza mahari yangu ninayotaka na sioni haja ya kukiuka kigezo changu kwasababu Kama ridhiki ipo ipo tu”.

“Kuna jamaa alileta posa lakini alivyopewa hill sharti la milioni kumi jasho lilimtoka, akalilia milioni tano nikamgomea. Huo ndio msimamo wangu ila msemaji Wa mwisho ni Muumba maana siwezi jua huenda kapuku akatokea tukapendana akaniopoa huko mbeleni.

Mrembo huyo asiyeisha vituko kwa mavazi yake ambayo yamempa jina na umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa amegeukia muziki wa bongo fleva ambao anafanya vizuri na wimbo wake Wa papa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.