Hakuna Msanii wa Kike Anaenipa Shida:Ebitoke

Msanii wa kike wa maigizo ya vichekesho nchini, Ebitoke amekiri kuwa hakuna msanii wakike yeyote bongo anaempa shida wala kuwaza kuwa anaweza kushindana nae kwa sasa kwa sababu yeye anajiamini na anajua kuwa hakuna anaeweza kumpita kwa kipaji.

Akiulizwa na bongo5 usiku wa kutolewa ka tuzo za sinema zetu ebitoke alisema “hakuna msanii wa kike anaenipa shida kabisa , sijamuona bado labda mimi mwenyewe”

download latest music    

Akiendelea kuongea, ebitoke pia alitoa taarifa kuhusu kuzushiwa kutoka kimapenzi na mdogo wake Ben Pol anaeitwa Wyce ambae ameweza kuwa video queen katika video yake mpya.

Hali ilikuwa poa, mimi na yeye tulikuwa tunavaaa uhalisia tu hakuna mapenzi pale,na kuhusu lile kiss hakuna kitu ila director alituambia tuvae uhalisia tu ili kitu kiwe kizuri.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.