Hakuna Msanii Wa Kumshusha Diamond Labda Afe- Baba Levo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na mwanasiasa, Baba Levo amefunguka na kumrusha msanii mwenzie wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai kuwa hakuna msanii yoyote anayeweza kumshusha labda afe.

Baba Levo ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwanga mkoani Kigoma kupitia chama cha ACT Wazalendo amemtukuza mkali huyo baada ya kuhaidi na kumpa zawadi Shilole ya kumtangazia bidhaa yake ya shishi chilli.

download latest music    

Siku chache zilizopita kwenye harusi ya Shilole na Uchebe iliyofanyika maeneo ya Mikocheni, Baba Levo ndiye alikuwa Mshehereshaji / Mc. Baada ya Diamond kumtaka Shilole kuchagua zawadi Baba Levo alivutiwa nakumwagia sifa kibao msanii huyo.

Kwenye maneno hayo na sofa hizo alizomwagia Diamond haya ni baadhi ya maneno aliyoyaongea:

Diamond Platnumz amehaidi kusapoti biashara yenu ya kuuza chilli nchi nzima na nje ya Tanzania jamani mimi naomba nimshukuru sana Diamond na hii ndio sofa kubwa ya watoto wa Kigoma na hii tafsiri yake ni kwamba huyu Diamond ni mkarimu kwani amekubali kukutangazia bidhaa yako bure buree na Shilole usingeweza kumlipa mama huyu ndio supastaa wa nchi alishashindikana tumejaribu wee sasa tumenyosha mikono acha atutangulie siku akifa na sisi tutapanda pale juu alipo kumzidi Diamond hatuwezi labda tumsubirie afe”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.