Hamisa Mobetto aandika ujumbe ambao umewaacha wengi wakijiuliza Kama mtoto anayemtarajia ni wa Diamond Platnumz

Hamisa Mobetto ameonyesha kuwa yeye hamuogopi mtoto yeyote ata Zari Hassan ambaye ni ‘mke’ wa Diamond Platnumz na mama ya watoto wake wawili.

Hii ni baada ya mrembo huyu kuandika ujumbe ambao umewaacha wengi wakijiuliza ikiwa mtoto anaye mtarajia ni wa Diamond Platnumz. Mrembo huyu aliandika kusema,

download latest music    

Mama Daa…? Mama dee…? Mama dii..? Mama doo..? Mama duh..?

Kulingana na mashabiki wa mrembo huyu, kuna unawezo kuwa Hamisa Mobetto alikasirishwa na video ambazo Zari aliwachia Jana kwenye Instagram yake – huku akionekana akitabasamu Diamond akimchezea gitaa wakiwa wawili huko Afrika Mashariki.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza ya Mobetto kufanya jambo kama hili kwenye mitandao yake ya Instagram. Ingawa hapo awali Diamond Platnumz alikuwa ameilana mimba hiyo….kwa hivi sasa hakuna uhakika nani anasema ukweli.

Tazama post hiyo hapa;

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua