Loading...

Harmonize Afungukia Sakata La Kuwatukana Wakenya

January 10, 2019 at 07:03
Harmonize Afungukia Sakata La Kuwatukana Wakenya

Staa wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rajab Abdul ‘Harmonize’ amefunguka na kuweka wazi Sakata lilimkuta siku chache zilizopita alipokuwa nchini Kenya.

Harmonize alifanya tamasha la Wasafi Festival Kenya tarehe 31 mwaka jana ambapo stejini aliwaambia Wakenya wanampenda kwa sababu Wakenya ni maskini wenzake ndiyo maana wanamuonesha mapenzi ya kweli katika muziki wake, lakini wao walitafsiri vibaya.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko Harmonize alisisitiza hakuwa na maana mbaya ila kilichotokea kilikuwa ni lugha gongana tu:

Unajua Kiswahili cha Wakenya na Watanzania ni tofauti ndiyo maana walitafsiri vile, ila mimi niliwaambia kwa nia nzuri tu kuwa watu wengi wananiuliza kwa nini Wakenya wanakusapoti sana kwenye muziki wako? Nikawaambia ni kwa sababu wao ni maskini kama mimi ghafla nashangaa watu wananishautia huku wanatikisa vichwa.

Huku wakisema usituite maskini maana tumelipa viingilio, sikutegemea kama itafikia hivyo, lakini nilitamani wajue kuwa sikumaanisha vibaya nawezaje kuwaita maskini wakati wao ndiyo wananiwezesha jamani”.

 

Share

Comments

  1. 😂😂😂😂

  2. wakenya hawataki upuzi huo wa kuitwa maskini 😂😂

  3. aisee utajipanga

  4. kenyans are a difficult people

  5. pole kwa yaliyokusibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…