Harmonize na Wolper Mapenzi Moto Moto

Msanii wa Bongo fleva nchini kutoka WCB Harmonize na msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper wamezidi kutengeneza headline kwa tetesi za kurudisha Penzi Lao Kama zamani.

Wawili hao wameendelea kuzua gumzo baada ya Harmonize kutangaza kurudi kwa Wolper wake ambaye alimwagana naye miezi kadhaa iliyopita. Ishu nzima ilijiri usiku wa kuamkia juzi Jumamosi katika shoo ya Wasafi Festival iliyofanyika mjini Iringa na kusababisha mji huo kutikisika.

download latest music    

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Wikiend iliyopita katika Uwanja wa Samora, Harmonize alimpandisha stejini Wolper kama ‘sapraizi’ na kumwangukia akimuomba warudiane, jambo ambalo Wolper alilikubali mbele ya maelfu ya mashabiki wao.

Naomba niseme wazi hapa hadharani kuwa nimerudi kwa Wolper wangu”.

Kufuatia kile kilichojiri mjini Mtwara ambapo Wolper alieleza nia yake ya kumrudisha Harmonize kwenye himaya yake ambapo wengi waliamini kuwa wawili hao wamerudiana maana wahenga walisema kiporo hakihitaji kupashwa na moto mwingi.

Pamoja na kuwepo kwa tetesi za wawili kurudiana Mpenzi wa siku nyingi wa Harmonize, Sarah ambaye kwa sasa yupo nyumbani kwao nchini Italy lakini amesema wazi kuwa yeye na mpenzi wake Harmonize bado wako wote na anategemea kurudi Tanzania muda wowote.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.