Harmorapa Amuomba Radhi Master J Kwa Upuuzi Aliomuongelea

Mwanaumuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka tena na safari hii amedai kuwa anamuomba msamaha producer maarufu Bongo Master J.

Harmorapa amemuomba radhi producer mkongwe bongo baada ya kudai kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia hapo kabla. Master J ni moja kati ya waanzilishi wa mziki wa bongo fleva kwa kuhusika katika kuvumbua vipaji vingi kupitia studio yake ya Mj Records.

download latest music    

Harmorapa alifunguka hayo alipokuwa anahojiwa kwenye kipindi cha Enews ya East Africa TV na kusema katika mwaka huu wa 2017 amemkosea sana Master Jay kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi cha nyuma kupitia katika kipindi hicho ambapo alidai kuwa hamjui wala hamtambui mtayarishaji huyo mkongwe wa Bongo fleva.

Kwa kweli niligundua kuwa nilifanya makosa makubwa sana, unajua kipindi kile nasema vile nilikuwa sijamjua vizuri Master Jay hivyo naomba anisamehe”.

Kipindi cha nyuma Harmorapa aliwahi kumkana mtayarishaji huyo wa muziki na kudai kuwa hamjui wala hatambui kipaji chake Harmorapa alitokwa na povu hilo baada ya kusikia Master J akidai kuwa Harmorapa hana kipaji chochote cha kuimba wala kucheza labada ajaribu fani ya uchekeshaji maneno yaliyomchoma Harmorapa kupita kiasi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.