Hemed PHD Adaiwa Kuwa Kicheche Bongo Movie

Msaniii wa filamu za Bongo movie na msanii wa Bongo fleva, Hemed Suleiman ‘PHD’ amejikuta ndani ya skendo nzito ambapo wasanii wenzake wamemnyooshea kidole kwa kuwa hajatulia na kuwa kiwembe.

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii wengi wa Bongo nmovie wamekuwa wakilalamika kuwa msanii huyo hajatulia kwani amekuwa akitembea na wengi wao kisha kuishia kuwatosa na hata kumtuhumu kwa kuringa na kujisikia.

download latest music    

Unajua wadada wengi wa Bongo Muvi, hasa mastaa wanampenda sana Hemed, lakini mara nyingi yeye anakuwa hana muda nao kabisa hivyo akiona wanamsumbua, anachofanya ni kutembea na staa kisha anambwaga wala hana muda wa kuendelea naye tena kwa sababu ana mwanamke ambaye amezaa naye na wanaishi wote,” kilisema moja ya vyanzo hivyo na kuongeza: “Sasa unaambiwa kuna mastaa ukiwatajia jina la Hemed hawana hamu naye kwa sababu walishatendwa na kuachwa solemba”.

Baada ya madai gazeti hilo lilimsaka Hemed ambaye baada ya kusomewa mashtaka yake hakusita kabisa kuanika ukweli wote;

Mimi sijawahi kumtaka mtu Bongo Muvi labda wenyewe ndiyo wananitaka, lakini siyo mimi ninawatokea wanakuja wenyewe na Mimi kazi yangu ninabutua, nasepa zangu halafu mimi sina mpango wa kutoka na staa wa Bongo Muvi”.

Lkaini pia msanii huyo ameweka wazi kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanamke mwingine ambaye hana ustaa bali ni mwanamke anayejiheshimu tofauti na wasanii wengi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.