Hivi Ndivyo Khadija Kopa Alivyowachamba Wasanii Wapenda Kiki

Malkia wa muziki wa Taarabu nchini Bibie Khadija Kopa amewajia juu na Kuwachamba wasanii wenzake wote wale wapenda kiki na kudai kama umaimba mziki mzuri na kuwafurahisha mashabiki wako hutahitaji kutumia kiki.

Wasanii wengi nchini sahivi wameingiwa na hiki kitu kinaitwa ‘kiki’ ambapo wanatengeneza bifu au skendo za uongo kwa maksudi kabisa ilimradi tu wapate attention ya mashabiki ili wakitoa kazi zao zipate airtime ya kutosha kwani watapata interview nyingi kutoka kwa waandishi wa habari.

download latest music    

Khadija Kopa amefunguka kwa kichambo hiko alipofanya mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi cha Enews ambapo amefunguka yafuatayo:

Hili suala la kiki linatokana na msanii mwenyewe anavyohisi labda wanahisi wakipata kiki zile za kuwa dhalilisha ndio watapanda zaidi kimuziki labda lakini mimi kitu sina na wala sipendi kwanza mimi mambo yangu binafsi napenda yawe ya siri na mambo yangi ya kifamilia napenda yawe ya siri na pia mambo yangu ya mahusiano au mume napenda iwe siri mimi mwenyewe, hasa nikiwa na bwana tuseme sio mums wa ndoa hiyo ndio kabisa napenda iwe siri zaidi kwa sababu sipendi kwani kitu cha zinaa sio kitu cha kujitangaza wala kujifaraghisha lakini kama mume unaweza lakini sasa sio ndio nipate kiki eti nimepigana na mume wangu watu wote wajue hapana huo sio umaarufu wala usanii wa maana”.

Lakini pia Khadija Kopa amewaasa wasanii wenzake kuwa Usanii wa kweli ni pale ambapo mwenyewe utajiamini unaweza ukafanya kazi watu wakaipokea na kukubali basi hauhitaji vitu vya ziada.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.