Loading…

Huu Ndio Ujumbe Wa Babu Seya Kwa Raisi Magufuli

October 11, 2017 at 14:13
Huu Ndio Ujumbe Wa Babu Seya Kwa Raisi Magufuli

Mwanamuziki Nguza Vicking au maarufu kama Babu Seya na watoto wake walifungwa jela miaka michache iliyopita amefunguka na kumwandikia barua Raisi Magufuli.

Babu Seya aliyefungwa kifungo cha maisha jela bila matumaini yoyote ya kutoka amefunguka na kumuangukia Raisi kwani ndio tumaini lake la mwisho.

Loading...

Katika barua hiyo Babu seya aliandika;

“Naomba mwambieni Raisi Magufuli juhudi zake nazisikia, Mungu azidi kumpa maarifa azidi kuliongoza vyema jahazi la Watanzania. Raisi huyu nimependa hekima zake nami namfananisha na mwandishi wa makala za kitabu cha Mithali na Mhubiri. Mwambieni raisi nimeweka akiba yangu ya tumaini langu la mwisho kwake. Mungu ndio mfalme wangu Wa kwanza awezae kumaliza msiba wangu huu wa kuishi kwenye kuta za gereza”.

Aliendelea kumlilia Raisi;

“Wa pili ni yeye John Joseph awezae kunitenganisha mimi na maisha ya gerezani, siipendi ndoto yangu ya kufia gerezani, naichukia Kama tawala ya herode pale Galilaya, Naumwa na huku hakuna makaburi mazuri ya kuzikia wafu wetu. Mwambie aje anisaidie nije nifie mikononi mwa Mama yangu. Siku ntakayotoka ndio siku ntakapolivaa joho la uchungaji na nitapita mitaani kulihubiri neno la Mungu mpaka jasho langu ligeuke damu…NATUMAI KATIKA MKONO WA BWANA NA NINATUMAI KATIKA MKONO WA RAISI JOHN JOSEPH halleluyah tutaonana madhabahuni”.

Comments

  1. Kosa alilofanya duh! nashindwa hata kusema

  2. Sidhani kama JPM atamsikia maana watu waliumizwa sana

  3. Mungu ampe nguvu ni mtihani tu

  4. Jela kama motoni unavunjika moyo kabisa

  5. Muombe Mungu atakusaindia kaka omba msamaha kwake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.