Inawezekana Alikiba Ameamua Kubadilika Kwa Hili

Akiwa kama moja wa wasanii ambao wamezoea kukaa muda mrefu hata mwaka kutaka interval ya wimbo mmoja mpaka mwingine,Alikiba ambae sasa hivi anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Seduce me’ ambayo imepokelewa vizuri sana na mashabiki anaonekana kujifunzaa na kuamua kuacha tabia hiyo ya kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo mpya huku akiacha mashabiki zake wakilalamika katika mitandao.

Alikiba ni mmoja wa wasanii ambao wamekuwa wakiwafanya mashabiki wake kusubilia kwa Muda sana mpaka kuwapa tena nyimbo mpya, ingwa ni msanii anaependwa na kila nyimbo anayoitoa huwa inapokelwa vizuri , lakin nadhani ni wakati wa yeye kubadilika na kuamua kuwaridhisha mashabiki wake.

download latest music    

kuna uwezekano mkubwa kuwa ni kweli Alikiba sasa amejirekebisha , hii inaweza kuthibitika baadaya msanii huyo kuandika katika ukurasa wake wa Instagram kuhusu ujio wa nyimbo mpya hivi karibuni.Akiandika kwa nia ya kumpongeza msanii mwenzie wa muziki wa Bongo fleva Abby Skillz kwa kufunga ndoa Alikiba, aliandika “Hongera mkongwe, nakutakia kheri na mafanikio  katika ndoa yako… Na ngoma mpya inakuja #SupportedbyKiba  #KingKiba ‘ alithibisha Alikiba.

Ingawa pia hii inaweza kuwa ni kama tishio kwa msanii mwenzie ambae wamekuwa na ushindani wa kimuziki kwa muda mrefu hapa nchini  tena hasa baada ya msanii huyo kutoa  wimbo mpya hivi karibuni, lakini pia huu ndo muda ambao pia Alikiba anapaswa  kuangalia zaidi mashabiki wake na kuendelea kutekeleza yale aliyowaahidi mashabiki wake , kwa sababu jinsi ambavyo namba kubwa ya  mashabiki walivyoupokea wimbo wake huu mpya vizuri  basi anapaswa kuendelea moto huohuo wa  kukonga nyoyo za mashabiki wake.Lakini pia kwa sababu hiyo ni ahadi , basi anapaswa kuitimiza ili kuendelea kutunza namba ya mashabiki zake lakini pia kuiongeza.

Kwa sasa Alikiba amekuwa ni moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika jukwaa la Fiesta , tamasha ambalo linaendelea nchini huku baadhi ya nyimbo zake kama ‘Seduce me’ ukiombwa kurudiwa kuimbwa zaidi ya mara tatu katika show moja, hii ni ishara nzuri ya upendo walionao mashabiki kwa msanii wao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.