Irene Paul Amkingia Kifua Muna

Msanii wa filamu za Kibongo, Irene Paul ameibuka na kumkingia kifua mwanadada Muna Love na kudai watu lazima waheshimu hisia za watu na kuweka mawazo yao pembeni.

Suala hili  limekuja baada ya sakata lililozuka jana baada ya Muna kufanya maongezi na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa Peter sio Baba wa marehemu Patrick na kumtaja Casto kama Baba Lakini pia aliweka wazi kuwa nyumba anayoishi Peter ni ya kwake na hati zote.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Irene Paul amemtetea Muna na kuwaomba watu wamuache aongee anachotaka kuongea kwani bado yupo kwenye maonbolezo ya mtoto wake.

Mimi nina mawazo kama walivyo watu wengine lakini ningependa tuheshimu hisia za Muna kama mzazi ambaye ni muhusika Mkuu wa mtoto aliyefariki na Kwenye maisha kila mtu ana jinsi ya ku-deal na stress kuna wengine wanapenda kuongelea matatizo yao na wengine wanapenda kunyamaza kwaiyo lazima tuheshimu mawazo ya watu”.

Kikao hiko cha Muna na waandishi wa habari hakikuaa vizuri na baadhi ya watu waliohisi ni mapema sana kuzungumza kwani mwanaye amekufa wiki mbili tu zilizopita na mmoja kati ya watu hao ni msanii Shilole:

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.