Irene Uwoya adhihirisha, kutokuchuja kwa ubora wake

September 13, 2017 at 15:31
Irene Uwoya adhihirisha, kutokuchuja kwa ubora wake

Mwanadada aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania  mwaka 2006 ambae pia kwa sasa ni msanii mkubwa katika tasnia ya filamu Irene Uwoya  amefunguka na kujipa sifa kubwa kuhusu kazi zake za sanaa.irene  anasema kuwa kipaji chake ni kipaji ambacho akiwezi kulinganishwa na mtyu yaani ni cha kipekee licha ya kuwa yeye ni mmoja kati ya wakongwe katika tasnia hii,kwa sasa hivi tasnia ya filamu imegubikwa na chipukizi la waigizaji lakini yeye bado anajiona kuwa ni mwamba hata kama kuna vitu vipya vinaibuka.

Irene anaongezea kuwa pamoja na udogo na uchipukizi aliokuwa nao kipindi hicho cha  mwaka 2008 lakini bado aliweza kutwaa tuzo ya  mwigizaji bora wa kike wakati ndio alikuwa bado mpya katika fani ya uigizaji kitu hicho  kinachozidi kumuongezea ubora wake katika kazi zake.”ubora wangu umedumu kutoka kuingia kwenye game  hadi sasa na hii yote ni kutokana na misimamo katika kazi,”aelezea Irene

Lakini pia irene anasema kuwa sio kwamba anaigiza kila filamu tu ilimradi ameigiza , na bado anaona kuwa yeye ndio msanii wa kike aliingia kwenye fani na kutwaa tuzo ya ubora.

Kuhusu yeye kuwa kimya ,Irene amesema kuwa kwa sasa ameigiza filamu moja tena imemlipa ela nyingi ivyo anasubiri iyo itoke ndipo aweze  kucheza filamu nyingine.

Hata hivyo, pamoja na uwepo wa skendo za mitandaoni kuhusu ugomvi wa yeye na baba mtoto wake ,na pia habari zilizokuwa zikisambaa kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na msanii mdogo wa Bongo Fleva  Dongo Janja ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha ngalenaro bado msanii huyo anaonekana kutokuteteleka na manen ya kwenye mitandao na bado anapeta na kujiamini zaidi.

Lakini pia kwa sasa hivi Irene uwoya amekula dili nono la kutangaza simu za kampuni ya Itel

Irene  Uwoya ni mama wa mtoto mmoja wa kiume  anaitwa ‘Krish’, mtoto ambae amezaa na aliyekuwa mume wake wa ndoa mcheza soka  Ndikumana lakini baadae walikuja kutengana.

Leave a Reply

5 Comments on "Irene Uwoya adhihirisha, kutokuchuja kwa ubora wake"

avatar
Sort by:   newest | oldest | most voted
Emanuel Ningu
Guest
Emanuel Ningu

uwoya kiboko ya wote

Salim Manga
Guest
Salim Manga

Yaan ww ni mkali kuliko hata yule Dada mlezi wa vijana kabisa

Lisa M
Guest
Lisa M

we ni Mdada Mrembo zaidi

Christopher Munge
Guest
Christopher Munge

Mbona umepotea sana

Aziz Abdul
Guest
Aziz Abdul

umependeza sanaa nipe namba tuchat basi

wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
wavatar

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.