Irene Uwoya Ajutia Ndoa Yake na Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya ameibuka na kuwashauri wanawake wasije wakaolewa na wanaume ambao mioyo yao haijaridhia.

Kama utakumbuka mwaka juzi Irene Uwoya alishangaza kila mtu Baada ya kufunga ndoa na msanii wa Bongo fleva Dogo Janja Lakini ndoa hiyo ilidumu kwa miezi michache na hatimaye kuvunjika.

download latest music    

Lakini hivi sasa Uwoya ameibuka na mapya ya kuiponda ndoa hiyo na Dogo Janja Kwa kudokeza kuwa aliolewa na Dogo Lakini kiuhalisia ni kwamba hakumpenda hata kidogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Uwoya alisema hiyo imewahi kumtokea akaolewa na mwanaume ambaye hakumpenda kitu ambacho kilimtesa hivyo wanawake wasiolewe ili tu waonekane nao wameolewa bali waingie kwenye ndoa na watu ambao wamewapenda kwa dhati.

Jamani wanawake wenzangu hakuna kitu kinachotesa kama kuolewa na mwanaume ambaye moyoni mwako hayupo, ni mateso makubwa hiyo ilishanitokea kwa hiyo nawasihi msijaribu kufanya hivyo kwani naamini ukitaka kuifurahia ndoa ni kuolewa na mwanaume unayempenda”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.