Loading...

Jacqueline Wolper Awachana Wanaume Wote ‘Wadangaji’

February 13, 2018 at 09:17
Jacqueline Wolper Awachana Wanaume Wote ‘Wadangaji’

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amewafungukia na kuwatolea povu wanaume wote ambao wanapenda kudanga.

Kudanga ni neno linalotumiwa sana hapa Bongo ambalo linaweza kumaanisha kuchuna buzi ambapo linawalenga hasa wadada wengi wa mjini ambao wanapenda miteremko katika maisha lakini sahivi mambo yamebadilika kwani hata wanaume wanatuhumiwa sana kwa kudanga.

Loading...

Wolper amewatolea uvivu wanaume wote ambao wana kawaida ya kuchuna wanawake zao ambao kwa hivi sasa ni maarufu kama vibeni-10, ambapo Wolper amewasihi wawe makini maana wakiendekeza kudanga basi wataishia kuwa mahouse boy.

Wolper alifunguka hayo na kurusha dongi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

Naomba mjifunze kitu wanaume wadangaji, mnadanga au mnadangwa mwisho wa siku unageuka houseboy kwa unayoenda kupambana nayo…..sio kila unachokiona kipo kama unavyokiona!”.

Baada ya ujumbe huo kusambaa mitandao ilianza kuenea kuwa hilo lilikuwa ni dongo ambalo Wolper alimrushia mpenzi wake wa zamani anaye julikana kama Brown ambaye alikuwa ni kiben-10 cha Wolper ambapo alikuwa analelewa na Wolper na kuhudumiwa kila kitu lakini baadae walikuja kuachana.

Wolper hivi sasa ana maisha mengine na ameshakuwa mchumba wa mtu baada ya kuvalishwa pete na mwanaume wake anayeitwa Engine ambaye ni msanii wa Bongo fleva.

 

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
JonesRisperDonDamarisOmbada Recent comment authors
newest oldest most voted
Ombada
Guest
Ombada

tell them

Damaris
Guest
Damaris

well said

Don
Guest
Don

kabisa

Risper
Guest
Risper

wanaume ni wale wale

Jones
Guest
Jones

word!


in Entertainment

Loading…

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.