Johari Adaiwa Kuwahi Kubanjuka na Petit Man

Msanii mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amedaiwa kuwahi kuonja Penzi la Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache.

Global Publishers wanaripoti kuwa waliwahi kubanjuka kipindi cha nyuma na hata juzikati walinaswa wakiwa kwenye uzinduzi wa filamu ya msanii Daud Michael ‘Duma’, Nipe Changu uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

download latest music    

Baada ya  picha ya wawili hao wakiwa pamoja Mlimani City kusambaa gazeti la Amani liliwatafuta na kufanikiwa kuzungumza na Johari huku Petit simu yake ikiita bila kupokelewa.

Jamani yule ni mshkaji tu na tukiwa karibu watu wanadhani tunatoka, sijawahi kutoka naye na sidhani kama ninaweza kufanya hivyo sababu ni mume wa mtu, naheshimu”.

Petit amemuoa dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz na pia Johari naye amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano na mwanamume mkoani Mwanza.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.