Jokate Awasihi Vijana Watumie Mitandao Ya Kijamii Kutafuta Fursa

October 12, 2017 at 12:59
Jokate Awasihi Vijana Watumie Mitandao Ya Kijamii Kutafuta Fursa

Mwanamitindo Jokate Mwegelo amewafungukia vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kuiona Kama fursa ya kuweza kuboresha maisha yao badala ya kutumia kwa udaku tu.

Jokate aliongea hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na Sam Misago ambapo alitoa ushauri kwa vijana ni kwa jinsi gani wanaweza kutumia mitandao ya kijamii kuboresha maisha yao.

“Nafikiri vijana watumie zaidi mitandao ya kijamii kuweza kujielimisha kwa sababu katika ulimwengu wa sasaivi kupitia mitandao ya kijamii tumeona kuna habari nyingi ambazo zinawekwa na pia kumekuwa na fursa nyingi sana kwa vijana kwa mfano kuibuka kwa biashara kama lebo kubwa tu za nguo za nchi za nje kwasababu tu wameweza kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa iyo Vijana waone mitandao ya kijamii kama fursa ya biashara isiwe sehemu tu ya kupiga umbea na udaku na kutafuta umaarufu ambao hauna faida”.

Jokate aliendelea kueleza umuhimu wa mitandao ya kijamii katika biashara;

“Mitandao ya kijamii tukiitumia vizuri inaweza kutunufaisha na tukaweza kumsaidia raisi wetu kutimiza adhma yake ya kuona Tanzania inakuwa nchi ya viwanda, kwaiyo vijana tupende kujifunza kwenye hii Mitandao tuitumie tu vizuri  kwa kunyanyuana zaidi ili tuzidi kuona fursa mbalimbali zilizopo kuliko kutumia kwa kupiga umbea na kufuatilia maisha ya watu binafsi”.

Jokate pia ni moja kati ya watu ambao ametumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kufanya biashara, Jokate ambaye ni miiliki wa kampuni inayotambulika kama ‘Kidoti’ ameweza kutumia mitandao ya kijamii kuitangaza na kuikuza biashara yake.

Leave a Reply

5 Comments on "Jokate Awasihi Vijana Watumie Mitandao Ya Kijamii Kutafuta Fursa"

avatar
newest oldest most voted
Patrick
Guest
Patrick

Anasema ukweli sio kila wakati kupost upuz

Wilson
Guest
Wilson

Vijana msipoteze fursa fungukeni macho

Esther
Guest
Esther

Ni opportunity nzuri sana

Maulid
Guest
Maulid

Yan dada nakupendea wosia mzuri sana

IBRAHIM
Guest
IBRAHIM

Asante sana Jokate


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.