Juma Jux afunguka kuhusu suala la kujiunga na Wasafi Records

Jux  ambaye ni msanii mkubwa bongo anaonekana kufanya vyema na wimbo wake mpya utaniua.

Hatah ivyo akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio msanii huyo alisema kuwa Wasafi record ni label nzuri lakini hajawahi kufikirikia kujiunga na label hiyo.

download latest music    

Ni kitu kizuri sio kibaya kwa sababu ile ni record label, hiyo nafasi ikipatika sio mbaya lakini kwa mimi sikuwahi kufikiria kwa hapa Tanzania au kwa Africa kwa kweli.

Hata hivyo yeye binafsi hana shida yoyote ya kujiunga na label hiyo iwapo watazingatia mkataba wake kwa sababu hafanyi muziki peke yake.

Iwe ni kampuni au sehemu ambayo itanichukua mimi kama kunimeneji pale nilipokuwa wafanye vitu extra zaidi. Sawa wanaweza ikawa wanaweza kwa mkataba kama watakuja na mkataba ambao nitautaka na vitu vyangu ambavyo navihitaji naweza nikasaini kwa sababu mimi ni mfanyabiashara lakini kwa sasa hivi hatukuwahi kuongea au kufikiria.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua