“Kamwe Siwezi Kufurahia Matatizo ya Sugu” Amefunguka Faiza Baada Sugu Kuwekwa Mahabusu

Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally ambaye pia anajulikana zaidi kwa kuzaa na Mbunge Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameongelea hali inayomkabili Mbunge huyo kwa sasa na kudai kuwa hawezi kufurahia matatizo yake.

Faiza na Sugu wamekuwa wakirushiana maneno mtandaoni mara kwa mara huku Faiza akionyesha wazi wazi chuki yake kwa mzazi mwenzake huyo huku akidai kuwa pamoja na wadhfa wake alionao serikali hamjali wala hamtunzi binti yao waliozaa wote.

download latest music    

Siku ya Jumanne Sugu alifikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka ya uchochezi ambapo ilidaiwa tarehe 30 December kwenye mkutano wa Chama Sugu alitia maneno ya uchochezi dhidi UA serikali.

Baada ya majanga haya kumkuta mzazi mwenzie Faiza kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo;

Kamwe sitoweza hata siku moja kufurahia matatizo ya Baba Sasha hata ikibidi kuandamana apate haki yake ningefanya hivyo! Matatizo yangu na yeye ni kimapenzi tu si vinginevyo na yaliisha mwisho wa siku ni baba wa mwanangu na wamefanana sana na mwanaye wamefanana hadi harufu zao kila ninapomuona namuona baba yake na nikifanya ubaya nitakuwa namfanyia mwanangu. All I wish Sasha na baba yake wawe hair na wawe na furaha so kama mnahisi nafutahia matatizo yake mpo very wrong kwa ufupi nimetafutwa na watu wengi wanasiasa na wanamziki iili nimchafue lakini sijawahi kiwapa nafasi nikiwasha moto ni kwasababu zangu binafsi na so kea kutumwa na by the way amelipa ada I hope atakuwa baba bora in future”.

Baada ya kifikidhwa mahakamani kea tuhuma hizo za uchochezi Dugu alitoa taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii na kuandika “Polisi wameniita wanipeleke mahakani kwa wanachodai uchochezi, Najisikia kama Nyerere  wakati wa ukoloni au Mandela wakati wa Uhuru”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.