Kim Nana Ajikanyaga Baada Ya Kuulizwa Kuhusu Penzi Lake na Tbway

Video queen maarufu kwenye tasnia ya Bongo fleva Kim Nana ambaye alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amejikuta akijikanyaga Baada ya kuulizwa kuhusu Penzi lake jipya.

Kwa muda wa Wiki chache sasa kumekuwa na tetesi kuwa Kim Nana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mtangazaji wa East Africa Television Tbway 360.

download latest music    

Gazeti la Risasi Jumamosi linaripoti kuwa Kim Nana kwa sasa yupo kwenye penzi jipya na mtangazaji huyo ambapo siku ya Valentine mwanadada huyo alimnunulia Tbway saa na mwanaume huyo alimpa viatu.

Mmhh! Vile viatu nimenunuliwa na mpenzi wangu siku ya Valentine ndiyo. Hapana siwezi kumtaja Mpenzi Wangu”.

Baada ya Kuulizwa kuhusu uhusiano wake  na Tbway Kim Nana alijikanyaga na kukata simu ambapo amekataa kabisa kuongelea mahusiano hayo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.