Lemutuz Aingilia Kati Sakata la Diamond na Baba yake

Moja ya watu maarufu katika mitandao ya kijamii Lemutuz amefunguka na kuingilia kati sakata la Diamond na baba yake ambalo linandelea katika mitandao ya kijamii , huku watu wengi wakimshambulia msanii huyo kwanini hataki kumsaidia baba yae ambae ni mgonjwa .

Lemutuz anasema kuwa watu wanatakiwa kujua kuwa Diamond ni mtu mzima hivyo anajua kile anachokifanya kwa sasa na kikubwa zaidi kutoa msamaha ni uamuzi wa mtu sio kulazimishwa.

download latest music    

Lemutuz anasema kuwa pamoja na yote , alichokosea baba wa diamond ni kuleta maswala ya kifamilia katika mitandao ya kijamii kwa sababu walitakiwa kukaa chini kama familia na sio kwenda katika mitandao.

Ikumbukwe kuwa baba huyo kwa sasa ni mgonjwa kitandani akisumbuliwa na vidonda miguuni,lakini pia wiki iliyopita dada mkubwa wa msanii Diamond alikuja akitokea nje ya nchi kwa ajili ya kumsaidia baba yake lakini pia kufanya usuluhisho wa matatizo yake.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.