Lulu Michael Mahakamani Tena Kwa Kesi Ya Mauaji Ya Kanumba

Malkia wa bongo movie Elizabeth Lulu Michael  atatakiwa kupanda mahakamani tena Oktoba 19 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza tena kesi ya mauaji inayomkabili.Lulu ambae anakabiliwa na kesi ya mauji ya bila kukusudia ya msanii mwenzie Steven Kanumba yaliyotokea mwaka 2012,April 7.

Nyota huyo wa bongo movie alifanya mauaji hayo ya bila kukusudia kwa msanii mwenzie ambae pia alikuwa nae katika mahusiano ya kimapenzi walipokuwa pamoja.Mauaji hayo yalitokea baada ya wawili hao   kutokuelewana kwao.Hata hivyo miaka mitano iliyopita ambapo Lulu aliapoanza kukabiliwa na kesi iyo alikubali kumuua Kanumba  bila kukusudia walikuwa nyumbnai kwa marehemu Sinza Vatican.

download latest music    

Elizabeth Lulu Michael alikamatwa na polisi  kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia mnamo April 2012,na kupelekwa katika kituo cha Osterbay.Baada ya kukamatwa na kuwekwa ndani  alikuja kupandishwa kizimbani katika mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar Es Salaam  ambapo hakutakiwa kujibu kitu chochote, na baadae kesi iyo ilikuwa kuwamishiwa mahakama kuu ili kusikilizwa tena.

Lulu alikuja akaachiwa kwa dhamana mwaka  2013, January  baada ya hati ya kesi iyo kubadishwa kutoka katika mauaji ya bila kukusudiana , hati ambayo ilimfanya apate nafasi ya kupata dhamana hiyo.

Steven Kanumba na Elizabeth Lulu Michael wote walikuwa na wasanii wa movie za bongo , Kanumba alikuwa moja ya wasanii wakubwa walisaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza kazi za movie nchini tanzania, katika kujibu tuhuma za kesi hiyo miaka minne iliyopita, Lulu Michael alikiri kuwa na mahusiano na msanii huyo na kuwa ni kweli aliua bila kukusudia.

Katika kujibu mashitaka yake, Lulu michael alieleza kuwa siku ya tukio alikwenda kwa marehemu Steven Kanumba  maeneo ya Sinza Vatican ambapo  walikuwa na ugomvi, hata hivyo hakusema bayana kitu kilichosababisha ugomvi huo.Lulu aliongezea na kusema kuwa katika purukushani na mpenzi wake huyo walivutana na alifanikiwa kutoka nje ya mlango lakini huko ndani kwa marehemu ambae alijigonga na kuanguka mambo hayakuwa shwari.Kila la kheri kwa malkia ya Bongo movie

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.