Mahakama yatoa muelekeo kuhusu kesi ya Wema Sepetu kukutwa na bangi

Muigizaji wa filamu ya Bongo Wema Sepetu amerejea mahakamani leo Agosti 18 kwa kuskizwa kwa kesi ya yeye kukutwa na bangi inayomkabili.

Siku chache zilizopita wakili wa upande wa washtakiwa (Wema Sepetu na wenzake wawili walioshtakiwa kwa kupatikana na bangi) na wakili wa serikali walikua na mvutano kwasababu ya ushahidi mpya.

download latest music    

Soma pia: Kesi ya Wema Sepetu yazua mvutano mzito

Leo hakukua na mvutano wowote katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba alitoa muelekeo kuhusu kesi hio ya Wema Sepetu.

Hakimu huyo alisema kesi hiyo imehairishwa hadi Agosti 31, mwaka huu ili kutolewa maamuzi, na tarehe 12 na 13 Septemba kesi hiyo kusikilizwa mfululizo.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere