Mama Kanumba: Wema Sepetu Ni Mwanamke Wa Kuoa

Mama mzazi wa marehemu Kanumba ambae alikuwa ni msanii mkubwa wa bongo movies  ambae safari yake ilikatika baaada ya kupata umauti baada ya kuuwawa na aliyekuwa mpenzi wake kipindi hicho Elizabeth Lulu Michael mwaka 2012, april 12.

Akizungumza katika Exclusive interview na waandishi wa habari wa kipindi cha Chilawadu kinachorushwa clouds Tv siku ya Ijumaa mama huyo alipata bahati ya kuzungumzia maisha aliyokuwa akiishi mtoto wake huyo kipindi cha uhai wake.

download latest music    

Akijibu swali aliloulizwa kuhusu ni wanawake wangapi Kanumba alishawahi kuwaleta nyumbani na kuwatambulisha mama kanumba alisema kuwa Kanumba alikuwa msiri sana na katika wanawake wote ni Wema Sepetu tu ndie aliewahi kutambulishwa na kuletwa nyumbani kama rafiki ingawa hakusema moja kwa moja kuwa ni mpenzi wake , lakini Wema alikuwa  msichana wa kuoa.

Katika wanawake wote  Kanumba alinitambulisha wema sepetu, na katika wanawake wote  wema alikuwa ni mwanamke anaepaswa kuolewa.Wema ni mwanamke alikuwa akija nyumbani akikuta unapika utaacha atapika yeye kama unaosha vyombo basi ataosha na alikuwa akija kwangu anakuja na madela.

Wema septu akiwa na marehemu Kanumba enzi za uhai wake.

Akiendelea kuongezea Mama Kanumba anasema kuwa hata katika baadhi ya interviews alizowahi kufanya kipindi cha uhai wa marehemu alikuwa akimwambia kila siku ukitaka kuzaa basi unapaswa kuzaa na Wema.Hata hivyo Mama Kanumba anaendelea kusema kuwa katika vitu anavyompendea wema ni kwamba yeye ni msanii wa kwanza siku zote kuongea kila siku  kuwa Kanumba ndio aliyemtoa.

Wema ni mwanamke ambae nilitaka kila siku aweze kuzaa na kanumba, yaani angezaa  na Kanumba ningefurahi sana.Yeye ni binti ambae siwezi kumlinganisha na binti yeyote yule kwa sababu alifundwa na akafundika kabisa achana na haya mambo ya sasa hivi ya kwenye mitandao.

Lakini kitu kingine ninachompendea Wema ni kwamba yuko straight forward sana,ni msanii pekee aliyewahi kukubali kuwa Kanumba ndie aliemuingiza katika sanaa.,

Mama Manumba alisema kuwa pamoja na kuwa wawili hao waligombana lakini hakuwahi kujua kuwa waligombana ingawa alikuwa akiona tu kwenye medias. lakini alitamani sana wema siku zote awe mkwe wake hao wenine yeye alikuwa hawajui kwakuwa kanumba alikuwa msiri sana.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.