Mama Wema Afungukia Mahusiano Ya Wema na Diamond

Mama Mzazi wa staa wa Bongo Movie Wema Sepetu, Mariam Sepetu amefunguka na kuongelea uhusiano wa binti yake Wema na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Wema na Diamond waliwahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu kwa miaka ya nyuma lakini tetesi za wao Kurudiana hazijawahi kuisha.

download latest music    

Katika interview aliyofanya na Gazeti la Amani, Mama Wema alifunguka mara baada ya mwanahabari wetu kumuuliza kama atakuwa tayari kupokea posa ya Diamond kama atajirudi na kuomba nafasi nyingine kwa bintiye, alisema wawili hao imebaki stori.

Wewee, sikiliza nikwambie bwana, Wema na Diamond kwa sasa wamebaki kuwa marafiki tu. Haiwezi kutokea tena wakarudiana. Mimi ndiyo namjua Wema vizuri, ana moyo wa aina yake ndiyo maana unaona pamoja na kuwa wameshaachana lakini bado wanakuwa karibu, wanashirikishana mambo yao kiroho safi.

Wema ana maisha yake sasa hivi, Diamond ana yake, kamwe hawawezi tena kurudiana“.

Hivi sasa itakuwa ngumu kwa Wema kurudi kwa Diamond kwani tayari Wema ana mpenzi wake ambaye amekwisha tangaza naye ndoa Lakini pia Diamond na yeye ana wanawake wake wengine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.