Martin Kadinda Afunguka Kuhusu Ugumu Anaopata Kufanya Kazi na Wema Sepetu

Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda ambaye pia ni meneja wa Msanii wa Filamu na Mwanamitindo Wema Sepetu amefunguka kuhusu changamoto anazopata kufanya kazi na mtu maarufu kama Wema Sepetu.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha East Africa Martin aliweka wazi kuwa anapata wakati mgumu sana kufanya kazi na Wema kwasababu hakui kimawazo kutokana na wakati unavyozidi kwenda. Amesema licha ya kuwa anampenda sana Wema na kuwa ni mtu muhimu kwenye maisha yake iwe kwa sababu ya kazi au bila kazi bado ataendelea kumheshimu   kwani tayari wana uhusiano mzuri sana.

download latest music    

Martin aliendelea kusema;

“Changamoto kubwa kwangu unajua Wema ni mtoto hakui, yaani miaka inakwenda bado yupo vile vile kikubwa ni kuweza kumtengenezea  mazingira ili kesho na kesho kutwa aweze kuheshimika. Unajua Wema ana maisha yake binafsi na vitu vyake anavyovipenda kwa hiyo ninachokifanya zaidi ni kuweza dhibiti mambo yake binafsi yasimfanye kesho na kesho kutwa kushindwa kupata ugali wake wa kila siku”.

Wema ni moja kati ya msanii anayependwa sana na Watanzania kutokana na Urembo wake lakini pia  ana kundi kubwa la mashabiki wanaojiita #teamwema. Hivi sasa Wema amejiingiza kwenye biashara zaidi ambapo anauza pia bidhaa mbalimbali za urembo pia hivi karibuni amefanya filamu yake mpya inayoitwa ‘Heaven sent’ ambayo inafanya vizuri sana sokoni

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.