Mbasha akataa kutelekeza familia

Msanii wa nyimbo za injili nchini  Tanzania Bwana Emmanuel Mbasha hivi karibuni alikutwa na kashfa iliyokuwa ikisambaa katika miatandao kuwa msanii huyo   ametelekeza familia mbili tofauti (wanawake wawili tofauti kila mmoja akiwa  na watoto)  amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa tetesi hizo ni uongo, na  hakuna kitu kama hicho na yeye hawezi kufanya hivyo,

Akiongea na mwandishi wa kituo cha televisheni cha  EATV , Mbasha amesema kuwa ‘ si kweli hivyo vitu ni vya uongo ,nakanusha kabisa hivi kwanini vitu vinaongelewa vya uongo alafu mimi sipendagi ” anaongea Mbasha na kuonekana kukataa kabisa kuhusu tabia ya watu kuzushia mambo yasiyo ya kweli.Hata hivyo Mbasha anasema kuwa tabia ya kuzushazusha vitu ni kutafuta kiki na ni mambo ambayo yanafanywa na watu wa  Bongo Fleva sio yeye muimbaji wa injili “huo  uongo uongo ni tabia za Bongo Fleva , mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelewa vitu ambavyo havina faida ” aliongezea Mbasha.

download latest music    

Tetesi hizo zinazo endelea kuenea katika mitandao kwa kipindi cha  hivi karibuni ni kuwa msanii huyu wa injili Emmanuel Mbasha amewzalisha wanawake wawili tofauti na kuwatelekeza na watoto wao nkisha yenyewe kujiingiza katika mahusiano na mwanamke mwingine inayesemekana kuwa yuko vizuri kifedha na ndiye anaemueka mjini msanii huyo.

Ni muda umepita sasa tangu  Mbasha  akabiliwe na kesi ya ubakaji, iliyomfanya kufikishwa  mahakamani ambapo baaada ya hapo alishinda kesi iyo dhidi ya mkewe aliyemshitakia,  mashataka hayo, baaada ya kesi iyo Mbasha aliingia katiak mgogoro mkubwa uliosababbisha yeye  kuachana na mke wake na  kupeana  talaka , mke wa Emanuel Mbasha ,Florah Mbasha pia ni msanii mkubwa na mkongwe wa injili nchini Tanzania  na kwa kipindi cha nyuma alitamba sana na vibao vyake kama ‘jipe moyo’ na ‘mwanamke simama imara’, wawili hao walipokuwa wakiachana tayari walikuwa wamepata  watoto wawili na walikuwa wakifanya pamoja kazi za muziki .Hata hivyo baada ya talaka Florah Mbasha alifunga ndoa na mwanamke mwingine huku akibaki na watoto wao wawili,

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.