Loading...

Mc Pilipili Alia na Wanaume Wanaomnyemela Mchumba ‘Ake

January 21, 2019 at 06:09
Mc Pilipili Alia na Wanaume Wanaomnyemela Mchumba ‘Ake

Mchekeshaji na Mshehereshaji maarufu Bongo Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ amekiri kuwa Penzi lake na mchumba ake Philomena Thadey ‘Cute Mena, linapumulia mashine kutokana wanaume kumtolea macho.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, MC Pilipili alisema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakimsumbua kila kukicha, hali inayomsababishia kukata tamaa.

download latest music    

Hawa wanaume walianza kumfuatilia mchumba wangu muda mrefu kabla hata sijaanza kumtangaza kwenye vyombo vya habari, lakini sasa wamezidi baada ya kumvisha pete ya uchumba.

Pia nimesikia kuna kijana eti yupo kwenye kituo kimoja cha redio (jina kapuni) naye anamfuatilia, nimebaki ninamuangalia tu kwa sababu wanaomfuatilia wapo wengi.

Kuna mwingine yupo Mwanza, mwingine yupo Mwenge, Ubungo, Mlimani City, Sinza, mwingine anatokea kampuni moja hivi ipo Posta, mwingine yupo Usalama wa Taifa na mwingine ni bodaboda sehemu f’lani hivi. Kwa hiyo mwisho wa siku inategemea na yeye mwenyewe kama wakimuingia, akawaelewa, basi nitamuacha aende, ikiwezekana labda hata uchumba pia naweza nikauvunja”.

Siku chache zilizopita Mtangazaji wa Choice Fm Mo J alikumbwa na kashfa ya aina yake Baada ya kusikika kwa taarifa kuwa alikuwa anamtongoza Mpenzi huyo wa Mc Pilipili ilhali yuko katika mahusiano na Gigy Money.

Loading…

Share

Comments

  1. eti uvunje uchumba na mke wako kwasababu anatongozwa? Una mambo

  2. huyu anapenda kulia kama mwanamke

  3. ukuiona ushaanza kuongea kuhusu kuvunja ndoa hapo basi kuna mambo

  4. pole

  5. At the end of the day hapa mwenye uamuzi ni mkeo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment