Loading...

Mc Pilipili Amtaka Ben Pol Amuoe Mpenzi Wake Mpya

January 08, 2019 at 08:03
Mc Pilipili Amtaka Ben Pol Amuoe Mpenzi Wake Mpya

Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili ameibuka na kumpa ushauri staa wa Bongo fleva Ben Pol wa kumtaka amuoe Mpenzi Wake Mpya.

Wiki chache zilizopita Ben Pol alianika mapenzi yake hadharani na binti wa Kikenya anayeitwa Anerlisa Mugai ambaye anatajwa kuwa mtoto wa kigogo na pia binti anayeogelea kwenye pesa.

Loading...

 

Mc Pilipili ameibuka na kutia neno kwenye mahusiano ya Ben Pol na Anerlisa ambapo  amesema watu wa kabila lake siku zote huwa wanapenda kweli kweli, hivyo akamtaka Ben Pol kuchukua maamuzi ya kuoa.

Wagogo tukipenda hua tunapotelea kabisa Ben Pol nakuelewa kaka yangu huu mwaka wetu kama tulivyoongea kaka”.

Mc Pilipili amekuwa kwenye headlines kwa siku mbili hizi Baada ya video yake alipokuwa anamvisha pete Mpenzi Wake na kuangua kilio  kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Share

Comments

  1. Kwa kuwa ana pesa au??

  2. Kaka Zetu mumeamua kupotelea nchi za nje kabisa

  3. Aoe haraka haraka amlete shemeji huku nyumbani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…