“Mimi na Zari Ndio Tupo Juu Wengine Wote Hamna Kitu”- Gigy Money

Video vixen na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameibuka na kudai staa pekee ambaye yupo kwenye level zake ni Baby mama wa Diamond Platnumz, Zari.

Gigy Money amefunguka hayo alipokuwa anaongelea trend yake ya kubadilisha Mawigi na mawiving siku za hivi karibuni.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Gigy amedai yeye na Zari ndio mastaa pekee ambao wanabadilisha nywele kichwani na wengine wote wanakuwa na tabia ya kurudia rudia nywele kichwani.

Yaani hao wanaojiita mastaa wengi Hawako katika level zangu maana sitaki kufanana nao ndio maana natumia pesa nyingi.

Hata wewe ukifatilia utajua mademu wanaobadilisha nywele kuna Zari na Gigy na labda nimuweke Irene Uwoya lakini kwa kuwa na yeye ni mtu wa siku nyingi namtoa lakini kwa sasa hivi ni mimi na Zari tu na tunavaa human hair hatuvai plstiki kabisa”.

Lakini pia Gigy Money amedai yeye ni kivutio cha taifa hasa mwili wake umekuwa kivutio kwa wengi ndio maaana anapenda kuchezesha mwili wake na ku twerk Kwenye shoo zake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.