Mimi Ninasema Wema Amekosea :-Steve Nyerere

Msanii Steve Nyerere amefunguka na kuongelea swala la Wema kuomba msamaha mbele ya waandishi wa habari baada ya kusambazwa kwa picha zake chafu katika mitandao ya kijamii akiwa faragha na mume wake mtarajiwa.

Steve Nyerere anasema kuwa yeye kama yeye anaamini kuwa Wema amekosea sana na anakubali kuwa waidhalilishwa kwa sababu wao i watu wa karibu na hata yanapotokea mabaya kama hayo wapo wanaokaa na kuwauliza kama wao wanafanya ninikumshauri wema mazuri.

download latest music    

Hata hivyo Steve anasema kuwa pamoja na kwamba amekiri na kuomba msahama lakini akae akijua kuwa kuna vyombo vikuba husika ambavyo vinaweza kukaa na kutafakari kosa lake , madhara yake na ukubwa wa kuomba msamaha wake na yeye hapo hawezi kuingila mamlaka husika.

mimi  sio mhukumu , mimi ni rafiki, kama ndugu wa karibu na jirani yake pia na ninasema kuwa Wema amekosea na amesimama kuomba radhi  lakini kuna vyombo kuna BASATA  kuna TAFF  na kuna wizara pia kama wizara na wao pia wamekaa kimya wanajitafaruku siwezi kuwasemea, lakini kwa upande wangu kweli wema amekosea na ametuomba radhi na ni kweli tulivuliwa nguo , hii ni kwa sababu watu walianza kuhoji kuwa hata wewe haukujamshauri.

Steve nyerere anasema kuwa wasanii wanapaswa kuwa makini sana wanapofanya jambo lolote kutokana na uwepo wa mitandao ambayo kila siku inakuwa na maendeleo ,hivyo kila kitu kinachoongelewa kwa sasa kinabaki mpaka kifo chao na bado yataendelea kuishi miaka na miaka.

lazima ifike muda tujitathmini kwa sababu haya yanayoonekana katika mitandao yanadumu mpaka tunakufa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.