Mnamuua Alikiba Mnapomlinganisah na Jux :-Chid Benz

Msanii  wa muziki wa kizazi kipya nchi wa siku nyingi , Chidi Benz amfunguka na kusema kwamba mashabiki na watu wa media wamekuwa wakikosea sana pale wanapotaka  kuwapaisha wasanii wasio na uwezo mkubwa na kuwaacha wale wenye vipaji vikubwa ni kibaya, kwani ni sawa na kumuua mtu.

Akiongea katika mahojiano na radio moja, Chid alitolea mfano kati ya wasanii wawili wa Bongofleva Alikiba na Jux, Chidi Benz amesema kwamba iwapo utampaisha Jux zaidi na kumuacha Alikiba, ni sawa na kumuua Alikiba kiakili, kwani wawili hao hawawezi kulinganishwa kulingana nauwezo mkubwa laionao Alikiba.

download latest music    

anasema “Jux sio msanii mkali, wanachomfanyia hawamfanyii hata Alikiba, mnamuua Alikiba kwa mawazo, mnachamnganya Alikiba kiakili, mnamtengua Alikiba kikazi, anakuwa anamuwaza waza Jux, watu wanamuangalia Jux, mnawaua waimbaji”, amesema Chidi Benz.

Kutokana na hilo Chid Benz amewataka kusapoti kazi za watu wenye vipaji kweli na kuacha kubagua kwa sababu yoyote ile, ili game iweze kukua zaidi na kuokoa wasanii wenye uwezo kutoanguka.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.