Msanii Adaiwa Kukimbia Ndoa na KuachaMadeni.

Msanii wa bongo movies Mkono wa Mkonole amedaiwa kuacha nyumba aliokuwa akiishi na mke wake kisa kuzidiwa na madeni na kuwa na maisha magumu tangu ameoa mwanamke huyo.

Mwanadada huyo ambae anasema kuwa alikuwa mke wa Mkono amefunguka hayo alipokuwa akiongea na eNews na kudai kuwa mume wake alimwandikia barua pindi alipokuwa ametoka na aliporudi alikuta barua hiyo kitandani huku yeye tayari akiwa ameshaondoka na kuelekea kyela kama aliyodai.

download latest music    

Hata hivyo mwanadada huyo aliejulikana kwa jina la sabrina ally anasema kuwa madeni yamekuwa mengi sana katika nyumba yao na ndio maana aliamua kuondoka huku akimuachia barau ayenye maelezo ya kutoka huku akisistiza kuwa hajamwacha mwanamke wake.

Mkono alindika hivi” sabrina mke wangu mimi ni mume wako fadhili, ninaandika barua hii nikiwa na akili zangu timamu,nimeamua kuondoka baada ya kuona kuwa tumekuwa na maisha magumu tangu mimi na wewe tumeoana, mimi nimeamua kwenda kyela kwa mjomba wangu kutafuta maisha  nikipata nitarudi mke wangu lakini sijakuacha”

Sabrina anasema kuwa ukiachana na madeni yote, mkono alikuwa na deni kubwa la benki ambalo dhamana ilikuwa ni hati ya nyumba ya baba yake hivyo anamuomba mume wake arudi na kushughulikia deni hilo kabla ya nyumba haijauzwa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.