Msanii Akothee Wa Kenya Matatani Kwa Uchafu Aliofanya Stejini

Msanii maarufu wa Muziki kutoka nchini Kenya Akothee amezua gumzo nchini humo siku chache zilizopita baada ya kufanya shoo ambayo alionekana alicheza kwa staili za ajabu stejini.

Akothee ameingia kwenye headlines nchini humo baada ya kutumbuiza kwa staili ya aina yake kwenye jukwaani la show ya Valentines Beach Party iliyofanyika Wikiendi iliyopita katika fukwe za Paparemo mjini Watamu nchini humo.

download latest music    

Akothee kama iliyowasanii wengine, alianza kuposti kwenye mitandao ya kijamii picha za show ambazo nyingi ziliashiria uharibifu wa maadili na kuchochea ngono kama wadau wa mitandaoni walivyomshambulia.

Lakini pia ishu hiyo imefika mbele zaidi Serikalini ambapo kupitia kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza La kuthibiti Filamu nchini Kenya (KFCB), Dkt. Ezekiel Mutua imelaani kitendo hicho.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.