Msanii Snura Mushi na Mpenzi Wake Wapata Ajali Ya Gari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko ya Mduara Snura Mushi ‘Snu Sexy’ pamoja na mpenzi wake Minu Calypto wamepata ajali ya gari siku ya jana mkoani Lindi walipokuwa anaelekea Kwenye shoo.

Taarifa za awali zinadai kuwa ajali hiyo ilitokea wakati Dereva wa gari la Snura alipokuwa anajaribu kulikwepa korongo na kusababisha gari hilo kupinduka.

download latest music    

Ndani ya gari hilo kulikuwa kuna watu watatno ambao ni Snura na Minu pamoja na madancer wawili wa Snura pamoja na Dereva wa gari hilo lakini kwa bahati nzuri kila mtu ni mzima zaidi ya majeraha machache.

Mpenzi wa Snura ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu ajali hiyo:

https://www.instagram.com/p/BmRRmsnFpXz/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rzkvn5quub6p

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.