Muziki wa Snura Watua Mikononi Mwa Snoop Dogg

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Snura Mushi maarufu kama Snu sexy amekula Shavu la haja  baada ya wimbo wake wa ‘Chura’ kurushwa na staa mkubwa duniani kutoka nchini Marekani rapper Snoop Dogg.

Snoop Dogg alirusha video ambayo inamuonyesha mwanadada akicheza wimbo wa Snura ‘Chura’ na kuonyesha kumvulia kofia.

download latest music    

Snoop ameiweka video hiyo Kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao una mashabiki zaidi ya Milioni 28 na mpaka sasa video hiyo imetazamwa na watu zaidi ya Milioni mbili.

https://www.instagram.com/p/BpBbq6eBPdT/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1758b5ns6v14b

 

Snura ameonekana kupata shavu nono kwani watu wameonekana kuikubali video hiyo na wimbo na hat wapo ambao wanaulizia muziki ule ni wa wapi na Watanzania wameendelea kumtag Snura.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.