Nabii Wa Uongo Atangaza Ndoa Kwa Wema Sepetu.

Nabii mmoja wa uongo anaepatikana mjini Dodoma maeneo ya Makulu na baadhi ya matawi ya kanisa lake yakiwepo jijini Dar Es Salaam ametangaza nia ya kutaka kumuoa Wema Sepetu ili waweze kuungana kwa ajili ya kuendeleza na kusambaza huduma za kanisa lake.

Nabii huyo ambae amekuwa akionekana katika mitandao ya kijamii katika video fupifupi akiwa ameshikilia bia na kitabu cha dini aina ya biblia amesema  kuwa Wema ni msichana mzuri kwa umbo na sura  na angetamani sana angekuwa mkewe kwa ajili ya kukuza huduma za kanisa lakini pia kuwepo kwa Wema katika kanisa lake kutafanya watu wajae kwa sababu watakuwa wanakja kumshangaa msanii huyo..

download latest music    

Wema ni msichana mzuri sana kwa sura hata umbo, nataka nimuoe ili awe mke wangu na  na awe sehemu ya kanisa lanhu piana nina imani watu watakuw wakijaa sana kanisani kwa sabau ya kuja kumuona yeye na wake zangu hawana tatizo na hilo kabisa na hata mmoja amekuwa akinisaidia kumtafuta na kuniunganisha nae.

Nabii huyo anaejulikana kwa jina la Tito, amekuwa akionekana katika mitandoa huku akiwa amevaliaa gauni jeupe lenye kuchorwa alama za misalaba miwili , ana wake watano na watoto 12 na amekuwa akihimiza katika mafundisho yake watu kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.

Katika kanisa la mzee huyo watu wamekuwa wakiruhusiwa kununua pombe na kuingia nayo kanisani huku akiwa na madai kuwa walevi ndio watakao uona ufalme wa mbinguni.Nabii huyo anaesemekana kuwa ni nabii wa uongo amekuwa akifanya mambo mengi ya kifuksa akiwa mbele ya watu .

Nabii huyo amekuwa akitembea katika ma-bar mbalimbali kwa ajili ya kutafuta waumini ambao ni walevi na kuwapa bia kisha kuwatolea mahubiri.Hata hivyo baada ya kusambaa sana katika mitandao ya kjamii  Nabii huyo anatakiwa kukamatwa kwa kosa la kuzaririsha wanawake kwa kile anachokuwa akikifanya  .

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.