Nandy Afunguka Baada Ya Kuwapa Wazazi Wake Nyumba

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka Nyumba ya vipaji Tanzania (THT)  Faustina Charles maarufu kama Nandy Amefunguka mara ya Baada ya kutangaza zawadi yake kwa wazazi Wake.

Siku chache zilizopita Nandy aliweka wazi Nyumba ambayo amewanunulia wazazi wake  Kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka kipande cha video na picha ambazo zinaonyesha nyumba hiyo na maelezo yanayosomeka:

download latest music    

“Mungu wangu na Baba yangu najua nakukosea sana kama binadamu na kama kijana ila nikipiga goti unajua namaanisha kutoka moyoni mwangu na unajua hakuna ninayemtegemea zaidi yako… Asante kwa kunipa uvumilivu, unyenyekevu, katika maisha yangu hasa kipindi hiki cha mwaka 2018!! Asante kwa hii zawadi ndogo ya wazazi wangu najua hii ni ndoto ya kila kijana mwenye kutafuta!!! Ni kila ndoto ya mwanadamu yeyote duniani kuona wazazi wake wako na furaha na ndiyo baraka zenyewe” .

Nashukuru media zote , blogs zote, ma producers wote, mapromoters wote, familia yangu ya THT, familia yangu ya clouds, management yangu, Team yangu, marafiki zangu, Baba yangu wa kiroho Mtumishi MWAMPOSA , na mafans wangu wote ,bila kusahau na hatters wote kwa kunipa nguvuu na supports kwa namna moja au nyingine uwepo wenu ndio mafanikio yangu……..
Nilijipa nguvu kabla sijapewa
Nilijipa moyo kabla sijapewa
Nilijiamini kabla ya kuaminika
Nilijikubali kabla ya kukubalika
Popote ulipo kijana mwenye ndoto yoyote ile jua inawezekana ukiweka nia ukikubali mazuri na mabaya yote yakufikie sababu ni daraja na nguzo ya mafanikio yako bila kusahau MUNGU ndiye kila kitu. Nawapenda
HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE ?
#DADAMWENYENYUMBA”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.