Nandy: Fedha Sio Kigezo Cha Mimi Kuwa na Uhusiano na Mwanaume

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ anayetamba na wimbo wake wa ‘kivuruge’ amefunguka na kudai kuwa ili yeye kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume sio lazima awe tajiri.

Wasanii wengi wa kike nchini wamewekwa kwenye kundi la wapenda pesa yaani ili umpate staa yoyote wa kike nchini ni lazima use na mkwanja mrefu. Wengi huita mapedeshee au madanga au sponsor ambapo baadhi baadhi ya wasanii wa like iwe ni wa Bongo movie au bingo fleva wanajulikana kwa kuwa na uhusiano na watu wanaojiweza kifedha tu.

download latest music    

Nandy alipofanya mahojiano na gazeti la Risasi vibes aliulizwa endapo kasumba hiyo mastaa wa kike kupenda wanaume wenye hela ina ukweli wowote alidai kuwa anachopenda yeye ni mwanaume mcha Mungu na mchapakazi haijalidhi kama hiyo kazi inamuingizia kipato kikubwa au la;

Kusema ukweli fedha peke yake sio kigezo cha mwanaume kuwa na mimi, muhimu mtu awe na hofu ya Mungu asiwe wa kujibweteka awe ni mtu wa kujishughulisha kwakazi yoyote ile tutapambana wote kutafuta maisha hadi mambo yatakapokuwa vizuri na kujivunia kwa pamoja kama wapenzi”.

Ingawa Nandy amekiri kuwa hawezi kuzungumza kwa niaba ya wanawake wote kwenye sanaa kuhusu nini matakwa yao lakini ameweka wazi kuwa wapo wanawake wa hivyo sehemu yoyote.

Nandy amekuwa katika vichwa vya habari kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Billnass ingawa wote wawili wamendelea kukana na kudai kuwa ni marafiki wa kawaida tu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.